Namna ya kupata watazamaji wengi kwenye blog yako bila kulipia shilingi
yeyote.
Kutengezeza blog ni
kazi rahisi sana ila kazi ipo kupata watazamaji. Wote tunajua bila
watazamaji hakuna maana ya kutengeneza blog. Unapoteneza blog unatakiwa ujue
mbinu utakazotumia kupata watazamaji.
Zifuatazo ni njia au mbinu zitakazokusaidia kupata
watazamaji wengi kwenye blog yako tena bila kulipa chochote.
1. Guest blogging hiki ni kitendo cha kuchangia
mada mbalimbali kwenye mitandao ya
wenzio halafu unaacha link yako kwenye maandishi yako. Unaweza weka link kwenye
neon au sentensi nzima ili msomaji akisoma atavutiwa kubonyeza link uliyoweka.
Angalia mfano kwenye ayah ii neon mbalimbali lina link ndani yake kwahiyo
ukiclick to utapelekwa kwenye mtandao wa mwandishi wa mada hii. Angalizo
usiache link nyingi sana hasa ukiandika mfano www.chatguest.com
link kama hii watu wengi wenye mitandao hawapendi kwani inajionesha dhahiri
lengo ni kuitangaza blog yako. Tumia mbinu ya hyperlink kwenye mfano wa neno mbalimbali
2. Comments: wengi tunajua maana ya comment hii ni
njia ya kuacha mtazamo wako kwenye blog post yeyote mfano baada ya kusoma
makala hii unaweza amua kuacha comment yako jinsi ulivyochukulia au kuielewa
mada hii kwahiyo ukisha andika maoni yako unajisajiri kwenye sehemu ya jina
yani NAME na sehemu ya Url unaweka link ya blog yako na mwisho unasubmit.